Alikiba Azungumzia Madai ya Kunyimwa tuzo ya MTV EMA na Kupewa Wizkid

Alikiba amefunguka kuzungumzia tetesi za kwenye mitandao ya kijamii kuwa amenyimwa tuzo ya MTV Europe Music Awards (EMA) katika kipengele cha Best African Act na badala yake tuzo hiyo kwenda kwa Wizkid.

Hatua hiyo imekuja baada ya muimbaji huyo wa Aje kuonekana kuongoza kwa kura nyingi zilizopigwa na mashabiki kupitia mtandao wa tuzo hizo.

“Kiukweli mpaka sasa hivi mimi mwenyewe sijui ni kwa sababu gani, watanzania na mashabiki wote hawajui ni kwa sababu gani. Kama ulivyozungumzia na juhudi zilivyokuwa zikifanyika pale na watu walipiga kura kweli, kwa sababu watu wanavyokuwa wakipiga kura pale mabadiliko yanakuwa yanaonekana,” amekiambia kipindi cha Jahazi cha Clouds FM.

“Kwa hiyo mashabiki walikuwa wanataka kujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea at least tuweze kupata hata voice ya explanation kiundani ili kila mtu afahamishwe ni kitu gani au ni vigezo gani wametumia kufanya mimi nisishinde ile tuzo. Hiko ndio kitu tunachosubiria na menejimenti yangu.”

Muimbaji huyo alikuwa akiwania tuzo hiyo pamoja na wasanii wengine, akiwemo Olamide na Wizkid kutoka Nigeria na Black Coffee na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini

Pata Nyimbo Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Mitandao Ya Kijamii
Facebook Fan Page: Bachema Tz
Twitter: @Bachema Tz
Instagram: @bachemaofficial
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment