Hili ndilo sharti ambalo Shilole amempa msanii wake ambaye anaishi naye..

Kama ulikuwa hujui Shilole kupitia kampuni yake ya Shilole Entertainment anamsimamia msanii mpya anayejulikana kama Gaucho.
Watu wengi wamekuwa wakitilia shaka huenda msanii huyo wa kiume akawa ana mahusiano ya kimapenzi na boss wake,Shilole kutokana na ukweli kwamba msanii huyo anaishi nyumbani kwa Shilole Lakini msanii huyo amekanusha na kusema kuwa Shilole amempa sharti la kutomtongoza.
Watu wanaongea sana kuhusu mimi na dada labda tunatoka kimapenzi,hilo suala ni hapana na pia kikubwa kinachochangia ni kuwa tunaishi wote na vile anavyoni treat ndio maana watu wanaongea lakini kipindi tuna sign mkataba aliniambia nikimtongoza ndipo mkataba wetu utakapoishia” alisema Gaucho ambaye kwa sasa ametoa wimbo wake unaoitwa Today.

0 comments: