Barakah Da Prince ajiunga na Rockstar4000 ambayo Yupo Alikiba na Lady Jaydee

Hitmaker wa Siwezi, Barakah Da Prince amesainishwa mkataba wa usimamizi na kampuni ya Rockastar4000.

Ameungana na Alikiba na Lady Jaydee kuwa msanii wa tatu kuwa chini ya uongozi huo. Na kwa sasa muimbaji huyo atakuwa akijulikana kama ‘Barakah The Prince.’

Kwenye maelezo yake, CEO na mwanzilishi wa label hiyo, Jandre Louw amedai kufurahishwa kumsaini muimbaji huyo wa Mwanza na kumwelezea kama mwenye kipaji cha hali ya juu.

Akiwa chini ya label hiyo, Barakah ataanza kuandaa album yake ya kwanza itakayotoka mwaka 2017.Muimbaji huyo amejipatia umaarufu kwa nyimbo zake kama Siachani Nawe, Nivumilie na Siwezi.

0 comments: