Director GQ: Wimbi la wasanii wa Bongo wa kufanya video nje ya nchi ni changamoto kwa directors.

Director GQ: Wimbi la wasanii wa Bongo wa kufanya video nje ya nchi ni changamoto kwa directors.
Director GQ kutoka Digital Vibe ya Morogoro aliyefanya video ya ngoma ya Belle 9, ‘Burger Movie Selfie’ ametoa neno kuhusu wasanii kukimbilia nje ya nchi kufanya video.
IMG_20160209_172821_042
Director GQ akiwa na @Kenedytheremedy
‘’Wasanii wa Bongo kwenda nje ya nchi kufanya video kwa sisi watayarishaji wa hapa nyumbani inatupa changamoto,kwa mimi inanifanya nifanye kazi zaidi sababu nijue kwanini msanii anaenda nje ya nchi kutafuta ‘production’ nzuri,’’ GQ.
‘’Sijajua kama kuna umoja wa Directors wa video kwa hapa Bongo,nadhani ni vyema tukakaa pamoja na kujua changamoto zilizopo na tufanyeje ili wasanii wabaki hapa nyumbani wafanye video zenye ubora,na kikubwa sasa hivi ninacho’focus’ nifanye kazi nzuri nihakikishe nina ‘connection’ na ‘outside’za kutosha.
‘Kwa sababu ukiwa tayari una ‘music video’ ambazo zinachezwa nje ya Tanzania na zinafanya vizuri basi msanii atakuwa na sababu zingine tu,lakini hapa hapa kuna directors wanatengeneza video ambazo zinapingwa nje ya nchi na zinafanya vizuri sidhani kama kuna msanii ataenda nje ya nchi kurekodi video, pia nafikiria kuzungumza na directors wa nje ili kupata ujuzi zaidi yuko jamaa yangu Australia nawasiliana naye’’GQ.
‘’Video ya Ali Kiba ‘Lupela’ ni nzuri amefanya kitu tofauti,mimi kama director nimejifunza kitu,’’ GQ.
SOURCE:CLOUDS FM
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment