Magufuli atangaza baraza la mawaziri,Ingia kuliona baraza lake...


rais dr john pombe magufuriRais wa Tanzania John Magufuli ametangaza baraza lake la mawaziri ambalo kwa sasa lina mawaziri 19, ingawa wizara ni 18. Mawaziri sita kati ya hao ni wanawake.
Dkt Magufuli amesema kuna nafasi nne za uwaziri ambazo bado anatafuta watu wanaofaa kuteuliwa.
Baadhi ya walioteuliwa ni:

Wizara ya Mambo ya Ndani- Charles Kitwanga

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa – Husein Mwinyi

Wizara ya Katiba na Sheria – Harrison Mwakyembe

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira – January Makamba

Wizara ya Ardhi – William Lukuvi

Wizara ya Mambo ya Nje na EAC/ Kimataifa – Augustino Mahiga

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na michezo – Nape Nnauye

Wizara ya Maji na Umwagiliaji – Prof Makame Mbarawa

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi – Mwigulu Nchemba

Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii – Ummy Mwalimu

Wizara ya Nishati na Madini – Sospeter Muhongo

Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu- Jenista Mhagama

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji – Charles Mwijage

Wizara ya ofisi ya Rais, Utumishi na utawala bora ina mawaziri wawili: Simbachawene na Kairuki

Wizara ya Sayansi, Teknolojia, Elimu na Ufundi Waziri – bado hajapatikana

Wizara ya Maliasili na Utalii Waziri – bado hajapatikana

Waziri wa Fedha na Mipango Waziri – bado hajapatikana

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Waziri – bado hajapatikana

Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment