Chukua Muda wako kumjua Director wa video za muziki kutoka South Africa, Justin Campos

Jina lake limepata umaarufu mkubwa sana kutokana na mikono yake kuhisika kwenye kazi nyingi za wasanii kutoka South Africa, Nigeria na sasa hivi Tanzania… Najua kuna watu wangu wengi wanalisikia sana jina la Justin Campos lakini hawamjui Justin Campos ni nani.
Kama wewe ni miongoni ya watu wanaopenda kutizama kazi nzuri za video production au kama wewe ni miongoni ya watu wanaovutiwa kutazama video za muziki zenye quality nzuri basi hii inakuhusu wewe moja kwa moja… Nimetembelea mtandao wa mseteoea na huko nimekutana na historia fupi ya Director Justin Campos, na nimeona itakuwa poa kama nikishare na watu wangu wengi ambao naamini jina hili sio geni masikioni mwao.
CAMPOS2
Justin Campos ni nani?
Safari ya Director wa video za muziki kutoka South Africa, Justin Campos kwenye Industry ya Entertainment ilianza mwaka 1994 alipoaanza kuandia ‘groove tracks’ kwenye studio, na kabla ya kufikisha miaka 17 Justin alikuwa ameshajitengenezea jina dogo kama  co-producer wa jingle za matangazo kwa wateja wa South Africa pamoja na wateja wengine kwenye soko la kimataifa… vyote hivi alivifanya kwenye studio ndogo aliyokuwa anamiliki pamoja na kaka yake D-Rex.
Justin Campos na kaka yake D-Rex walifanya kazi nyingi chini ya studio yao ikiwa pamoja na kupata deals kibao za kutengeneza soundtracks kwa ajili ya Nokia, Fanta, na McDonalds… baada ya kupata mafanikio, Justin aliamua kufuata ndoto yake ya siku nyingi ambayo ilikuwa ni video production/directing pamoja na kufanya production kwa ajili ya matangazo ya kibiashara.
CAMPOS
Kipaji chake na uwezo wake wa kutumia ‘special effects’ kwa ajili ya kuedit na kuongoza videos za wasanii wa underground kilikuja kugundulika na Record Execs ambao walisaidia kumkuza Justin kibiashara kwa kumpatia fursa nyingi zilizosaidia kuboresha uwezo na kukuza kipaji chake.
Baada ya kuiva vizuri chini ya Record Execs, Justin Campos aliamua kujaribu fursa za juu zaidi kwenye entertainment kwa kutengenza videos zenye ubora wa hali ya juu na hapo ndipo kampuni yake ya ‘Gorilla Films’ ilipozaliwa, na kuanzia kipindi hicho, Justin ameendela kukuza jina na umaarufu wake kwenye industry ya Entertainment South Africa na nchini nyingine za Africa ikiwemo na Tanzania ambapo baadhi ya wasanii wetu wametokea kupenda sana kufanya kazi na Director huyo.
Jina la kampuni yake ‘Gorilla Films’ linatokana na neno ‘Guerilla-filmaking’.
CAMPOS4
Wajue baadhi ya wasanii ambao kazi zao zimewahi kuguswa na mikono ya Director Justin Campos:
List ya wasanii waliopita kwa Justin Campos ni ndefu sana na pengine kuwataja wote itakuwa ngumu… lakini baadhi ya wasanii ambao kazi zao zimeshawahi kupita kwenye mikono ya Director huyo (wengine zaidi ya mara moja) ni pamoja na kazi za…
 1. UHURU – South Africa.
 2. Kabelo – South Africa.
 3. Oskido – South Africa.
 4. Kalawa – South Africa.
 5. Ntando – South Africa.
 6. Liquid Deep – South Africa.
 7. Runtown – Nigeria.
 8. Jux – Tanzania
 9. Vanessa Mdee – Tanzania.
 10. Joh Makini – Tanzania.
 11. Navy Kenzo – Tanzania.
 12. Shaa – Tanzania.
Kila ndoto inawezekana ukiamini na ukiwekeza jitihada kubwa kwenye kuzifanikisha ndoto hizo mtu wangu!
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
  Blogger Comment
  Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment