Ujerumani ikitinga Fainali kwa ushindi wa bao 7-1 dhidi ya Brazil huku Miroslav Klose akivunja rekodi ya magoli Duniani.


Miroslav Klose amefunga bao  la pili dakika 23 baada ya kuukuta mpira uliopanguliwa na kipa Julio Cesar kufuatia shuti lake mwenyewe na kuandika bao lake la 16 kwenye Fainali za Kombe la Dunia akiweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye fainali hizo, akimpiku Mbrazil, Ronaldo Lima… baada ya kuwafumua wenyeji, Brazil mabao 7-1 katika mcheo wa Nusu Fainali uliofanyika Uwanja wa Mineirao mjini Belo Horizonte, Brazil..Julai 08,2014.

  Ushindi huo unawafanya Ujerumani kufuzu Fainali ya Kombe la Dunia 2014,  kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12- mara ya mwisho ilifungwa na Brazil katika fainali zilizoandaliwa kwa pamoja na Korea Kusini na Japan na sasa watamsubiri mshindi wa leo (Jumatano Julai 09,2014) kati ya Argentina na Uholanzi.
Hadi mapumziko, tayari Ujerumani walikuwa mbele kwa mabao 5-0 yaliyofungwa na Toni Kroos mawili, Miroslav Klose, Thomas Muller na Sami Khedira.
Brazil ilionekana wazi kuathiriwa na pengo la kuwakosa wachezaji wake tegemeo, beki na Nahodha Thiago Silva anayetumikia adhabu ya kadi za njano na mshambuliaji Neymar ambaye ni majeruhi, ambao nafasi zao zilizibwa na Bernard na Dante.
 
Ujerumani ikafunguka tena na kwenda kufunga mabao mawili zaidi, yote Andre Schurrle aliyeingia dakika ya 58 kuchukua nafasi ya Klose akimtungua kipa Julio Cesar dakika ya 69 na 79.

Top five World Cup goalscorers

Position Name Country Goals Matches Played Goal Average Tournaments
1 Miroslav Klose Germany 16 23 0.70 2002, 2006, 2010, 2014
2 Ronaldo Brazil 15 19 0.79 1998, 2002, 2006
3 Gerd Muller West Germany 14 13 1.08 1970, 1974
4 Just Fontaine France 13 6 2.17 1958
5 Pele Brazil 12 14 0.86 1958, 1962, 1966, 1970
Brazil wakafanya shambulizi na kushitukiza na kujipatia bao la kufutia machozi lililofungwa na Oscar dakika ya 90.
Wachezaji na mashabiki wa Brazil waliangua vilio baada ya mchezo huo, huku Wajerumani wakiangusha pati la maana uwanjani.

"Manuel Neuer is surely the best goalkeeper in world football."
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment