DIAMOND ATUSUA TENA BET..NI HISTORIA NYINGINE KWA DIAMOND...


Katika jambo lililotokea kama suprize flani hivi, kwa mara ya kwanza katika historia ya muziki wa bongo fleva, nyimbo ya Diamond Platnumz “Mynumber1″ ilienda hewani jana kupitia television hiyo ya kimataifa ya BET, DiamondPlatnumz anaweka historia mpya tena kuonekana katika kituo hicho cha television, ikiwa haijawahi kutokea kwa mwanamuziki yeyote kutoka bongo kufikisha nyimbo yake level hizo na kufanikiwa kupigwa katika kituo hicho cha television kinachoangaliwa na maelfu ya watazamaji duniani kote. Diamond Platnumz amefungua pazia kwa dunia kuanza kuangalia vipaji vingine kutoka tzee, ikiwa huu ndio mwanzo tu wa mafanikio, akiwa ndiye msanii anayeongoza na kufungua kila njia ya historia mpya ya muziki wa bongo fleva.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment