DAKTARI MWINGINE FEKI AKAMATWA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO


Askari Polisi wakimtoa nje daktari feki, Karume Habibu (22) kutoka kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alihojiwa kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi.
Daktari feki akielekea kwenye gari.
Daktari feki, Karume Habibu akiingizwa kwenye gari.
...Akificha uso kukwepa kamera za GPL.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wakishuhudia tukio hilo.
WIMBI la madaktari feki kuingia katika hospitali wakijifanya madaktari na kutoa huduma mbalimbali limeendelea ambapo leo amenaswa mwingine mkoani Morogoro.
Daktari huyo feki aitwaye Karume Habibu (22)amenaswa katika HospitAl ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa mahojiano zaidi.
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)

0 comments: