WADADA WALIOKUWA WANAFANYISHWA BIASHARA YA NGONO CHINA WARUDISHIWA PASSPORT ZAO

Wiki iliyopita kupitia kipindi cha XXL na Gazeti la Makorokocho online niliweka hewani ule waraka wa wazi wa sauti uliosomwa kutoka China na Mwanadada Candy kwa niaba ya Wanadada wenzake wa Kitanzania walikua wakilalamikia kushikiliwa kama watumwa na kufanyishwa biashara ya ngono kwa lazima, waraka ule ulikua maalum kwa wizara ya mambo ya nje na watanzania kwa ujumla kwani kinadada wale walikua wakiomba msaada warudishiwe Passport zao zilipokonywa na watanzania wenzao, Binafsi Candy anashikiliwa nchini china tangu December mwaka jana,
sasa kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika ni kwamba Candy na Wenzake wamerudishiwa Passport zao ila simu zao za mkononi wamepokonywa, Candy anawashukuru watanzania wote kwa kuonyesha kuguswa na kwa vyombo vya habari kwa kuweka hewani waraka wao, na sasa hivi wako wanatafuta shughuli za kufanya kwani zipo nyingi sanaaaa China.
- See more at: http://www.makorokocho.co/2014/04/hatimaye-wadada-waliokuwa-wanafanyishwa.html#sthash.ZFu8H0Fx.dpuf
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment