ZITTO:NAMSUBIRI FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI

Mbunge wa kigoma kaskazini zitto Kabwe (Chadema), amesema anamsubiri mwenyekiti wa chama hicho, Freema mbowe mahakamani.
Zitto ametoa kauli hiyo baada mbowe kutangaza kumburuza mahakamani kutokana na kile kinachodaiwa kumzushia tuhuma za uongo
Nasema sitaki malumbano na kiongozi yoyote, nachotambua masuala ya mahakama yanajibiwa mahakamani na si vinginevyo" alisema zitto.

Zitto alitoa kauli hiyo, baada ya MTANZANIA kutaka kujua msimamo wake kutokana na kauli ya Mbowe kukududia kumshitaki, kutokana na madai ya kusema uongo dhidi yake. Zitto ambaye yupo nchini Nigeria anakohudhuria vikao vya kamati za Bunge za serikali kwa nchi za Afrika, alisema pamoja na Hali hiyo mahakama ndio njia pekee ambayo haki ya mtu inaweza kupatikana.
Alisema kwa msingi huo, hivi sasa hayuko tayari kuruhusu malumbano ambayo Hayana tija kwa Taifa.

" nipo Nigeria na bahati mbaya ninaumwa sana, ila hivi Leo ninamshukuru Mungu nimepata nafuu kidogo. Kama nilivyosema mwanzo sitaki Malumbano na mtu. Pamoja na kusema anaumwa, hakuwa tayari kufafanua ni ugonjwa gani unaomsumbua.

" huu muda nahitaji kutafakari maisha yangu kisiasa na kwa vyovyote vile masuala ya mahakamani yatajibiwa mahakamani", alisisitiza zitto

Nukuu gazeti la MTANZANIA la ZITTO KABWE ndio ICON ya Chadema ndio chanzo cha kupata nguvu kwa Chadema huwezi kutenganisha Chadema na Zitto labda kwa Kabila la wachaga ambalo kwao UKABILA wameweka MBELE, ndio MKOMBOZI wa makabila mengine ndani ya CHADEMA.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment