PETER MSECHU UMELALA SANA HUKO UNAPOELEA SIO-SOMA BARUA YA WAZI KWAKO

By Kinye Wynjones

Wanasema anayekutakia mafanikio atakueleza ukweli, hata kama ukweli utauma kiasi gani, as long as ni ukweli basi ukichukuliwa vizuri ni dhahiri kwamba utaleta matokeo chanya. Hii naandika kama shabiki ambaye nimekuwa nikikufuatilia kwa kipindi kirefu sana, tangu usaili wa BSS 2009 mpaka leo hii umeachia wimbo unaitwa FIRE japo sifa zako nilizisikia kabla ya hapo kwakuwa mimi na wewe elimu yetu ya sekondari tulisoma kwenye mji mmoja, nilikutangulia na niliacha kumbukumbu nzuri pale hivyo hata siku ulipotembelea shule niliyosoma wapo walionipigia simu kunikumbuka baada ya kazi uliyofanya pale kufanana na niliyokuwa nikiifanya.

Natafakari uwezo wako kimuziki na kusikitika kidogo. Wewe ulitakiwa kuwa muimbaji mwenye wafuasi wengi sana hapa Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla kutokana na majukwaa uliyowahi kuyapanda kwa ajili ya kutoshana nguvu na wengine na jinsi ulivyowachachanya kwa vipindi tofauti.

Nafasi ulizopata kama ungezitumia vizuri naamini leo hii ungekuwa hushikiki, sijui mipango yako ikoje katika kuteka soko, nimekuwa mvumilivu nikiamini lipo kubwa la kusubiriwa lakini it has been a long wait na ni kama nakata tamaa sasa haswa kila nikisikia umetoa wimbo.

Kujulikana ni silaha moja muhimu sana kwa kila msanii, bahati nzuri wewe tayari unajulikana sana. Baada ya kujulikana kuna mawili, its either kupendwa au kuchokwa na vyote have a lot to do with what u deliver to the audience “matoleo” kwa wewe kikubwa ni nyimbo, je ni zile zinazowafanya wakukubali na kukuongezea nafasi zaidi ama ni zile zinazowapukutisha kila leo kutokana na kutoridhishwa na kile uwapatiacho?

Kama walivyo wengi, mimi siridhishwi na mahali ulipo kwasababu najua una uwezo first class wa kudeal na huu muziki, sijui kama hii ni ‘rescue mission’ lakini naamini nguvu ya maoni yangu juu ya wewe japo si ya kitaalamu saaaana, hata kama wewe utadhani hayakugusi moja kwa moja yatakuwa ya msaada kwako endapo utayatilia maanani.
Kuna mengi yanayomkamilisha msanii, lakini mimi naamini katika muziki mzuri kuwa ni kitu cha muhimu sana kwa mafanikio ya msanii. Wewe unafanya muziki lakini naona siku hizi hauko serious kwakuwa kuna makosa madogo lakini ‘pricey’ unayoyafanya.

Vinavyokuangusha

Ad-libs zisizo na ulazima. Haya ni maneno ambayo huimbwa pasipo kuandikwa, mategemeo ni kuweka hisia nzuri ama kionjo maridhawa lakini kwako msechu there is too much adlibbing in your songs na ukweli ni kwamba zinaondoa utamu ama mashiko ya nyimbo zako kwakuwa nyingi huwa hazikai, kila wimbo wako ninaosikiliza nakutana na kero hii sehemu.
Kupayuka. Kitu ambacho siwezi kubisha ni kwamba una sauti nzuri tena ya pitch ya juu sana, hiyo ni strength yako na kwenye baadhi ya nyimbo imekuweka vizuri sana, ukisikiliza Majaribu bila shaka hata wewe mwenyewe unajikubali. Siku hizi ni kama una over do, umekuwa unapayuka hivyo kuondoa hata utamu wa nyimbo, nakusikiliza kwenye Kibudu nakereka, mwenyewe najiambia kuwa ulimpania sana Ally Nipishe. Intro ya wimbo wako “naogopa kupenda” pia umepayuka na sehemu nyingine nyinginyingi.

Sifa. Nisamehe kama neno hili ni kali sana, nakosa neno zuri la kuelezea kitu hichi kinachokuangusha. Msechu sijui huwa “unapoteza” ama “unatekwa” na kujisahau? Una sifa sana Msechu haswa wakati unaperform, lakini jinamizi hili linakuanda hata kwenye uimbaji, una changamka kupitiliza hivyo kujisahau wakati mwingine na kupoteza maana ya wimbo ama ladha ya wimbo.

Freestyle. Nijuavyo mimi ni kwamba wewe ni miongoni mwa waandishi wazuri sana lakini kuna maneno kwenye nyimbo zako nyingi naamini kuwa yanakutoka tu wakati unarekodi.Naliita tatizo kwako kwasababu ni la muda mrefu na hutaki kuliacha, nakumbuka 2010 ulipewa onyo hili na mmoja wa judges wa TPF, ndio una kitu wasichonacho waimbaji wengi lakini wewe unakiover use, nasikiliza wimbo “Kenya Itadumu” na kusema kwamba hukuwatendea haki Wakenya…wewe una uwezo zaidi ya pale, ni wewe ulitakiwa kuwafanya wausahau wimbo wa nguli wao Eric Wainaina “Daima Mkenya” ambao uko deep mara mia zaidi ya wako wakati uwezo unao tele Msechu.

Aina ya muziki. November 2013 ulitweet kitu kuhusu wimbo wa NAy wa Mitego “nakula ujana”, nakumbuka uliandika “Unakula ujana au ujana unakukula wewe? Utaimba hadi bolingo mwaka huu…kweli hiphop haiuzi…bado kidogo utakuwa dancer wangu Msechu Band….” Uhuru wa maoni ni haki ya kila mmoja na sikuzuii kutoa maoni yako, kilichonipa maswali ni kwamba wewe unafanya genre gani ya muziki? Huna consistency katika aina ya muziki ufanyayo, jana umetoa r n b, kesho zouk, leo rhumba…what are you trying to prove? Wewe unatakiwa kuwa na identity, kwamba tukimzungumzia PM basi tunazungumzia Muziki fulani.

Producers wako. Najua kila msanii anapenda kufanya kazi na mtu ambaye yuko huru naye lakini pia mtu ambaye wanachemistry nzuri. Wewe tayari umeshafanya kazi na producers kibaooo kitu ambacho kina madhara makubwa kwenye mziki wako kwani wengine hawana kiwango cha kukufanya wa kimataifa. Mimi ningekuwa wewe kuna nyimbo ambazo nisingethubutu kuziachia, nawajua wenzako kadhaa walio makini sana katika hili, nyimbo zisizo na kiwango wao huziita DEMO, na zinakuwa tayari kurudiwa…sasa wewe kinachosound kama demo kwako kimepita. Nakushauri usikilize nyimbo zako zooote na baadhi ya watu kisha msaidiane kuchakua producer anayekufaa zaidi, mimi ninaye kichwani tayari.

“Kutekwa”. Nashawishika kusema kwamba wewe huwa unawasikiliza na kuwakubali sana waimbaji mwingine na hatimaye kuwa carried away. Kuna baadhi ya nyimbo zako nikisikiliza moja kwa moja najua inspiration inatoka kwenye wimbo gani mwingine. Sio kitu kibaya kuwa inspired, ila sio kitu kizuri kwa mtu wa kiwango chako kutekwa. Ukidumu ulikujaa tele ila mashukuru Mungu imefikia hatua umeukwepa, wimbo “Kumbe” licha ya kuwa one of my favourites lakini nilikereketwa pindi nausikiliza, na haikuwa kauli yangu pekee bali ya wengine pia kwamba unaanza kwa kuimba kama Rama Dee kabisa.

Vitu hivyo hapo juu vinatokea kwenye nyimbo zako, na vingine vinajirudia, nashawishika kusema sikuhizi unafanya muziki kimazoea, unafanya muziki kwa kukamia, na zaidi unafanya muziki ukiamini wewe ni boooonge la nyota kitu ambacho ni ndio na sio. Hembu tuangalie nyimbo zako hapa kwanza kulingana na jinsi ulivyoziachia.

Viwango vya Nyimbo zako

HASIRA HASARA

Hapa hukuwa umekomaa sana kisanaa lakini ulidhihirisha ubora wako, hukutuangusha ndugu yangu japo, uliwaaibisha wengi, hususani wale ambao hawakuwa kwenye timu yako BSS, u proved them wrong na mpaka leo wewe ndio mshindi wa wengi wa mwaka ule japo hukuvikwa taji. Wimbo huu ninaupa NYOTA 4.

MAJARIBU

Ulibadilika sana humu ndugu yangu, ilinichukua muda kujua kwamba ulikuwa wewe, ulisound so professional and developed. For me this song is the best ever done by you japo wengi hawaujui kwasababu uliutelekeza, that song needed a video bruv!!! Hapa ulikuwa kimataifa kabisa, modern beat ikiwa na mitambao ya Kiafrika huwa inapendeza sana, If I were you I would stick to that genre. Wimbo huu ninaupa NYOTA 5.

UNANIUMIZA ROHO

Ulizidi kuonyesha ukomavu hapa, utofauti wake mkubwa na majaribu ni utengenezwaji, kwenye majaribu ulisound vizuri zaidi ila zote ni production matata, hii pia hukuitilia maanani sana akini ingekufikisha mbali. Ninaipa NYOTA 4.

RELAX

Nadhani relax ndio wimbo maarufu kuliko nyimbo zako zote. Wengi walikupenda humu lakini mimi hapa ndio nilianza kukuangalia kwa jicho la wasiwasi kwamba huyu jamaa anaelekea wapi? TPF ilikupa umaarufu sana na ulikuwa kichekesho (kwa maana nzuri) kwa wengi, ulikuwa chalechale sana na ukachangamka zaidi, uchangamfu ule uliuhamishia kwenye nyimbo zako kitu ambacho mimi nilikipokea vibaya, kuna vimaneno visivyoendana nawe ukavianza hapa, adlibs tele na video haikuendana nawe. Licha ya umaarufu wa wimbo huu mimi ninaupa NYOTA 3.

NAOGOPA KUPENDA

Sijui nani alikushauri kuachia wimbo huu, nakumbuka wakati unauachia nilipata nafasi ya kuuchambua nikiwa na wenzangu kwa ajili ya blog ya leotainment ambayo ilikuwa na segment ya postmortem kila ijumaa, wote tuliuponda kwa kiasi kikubwa japo hatukuwa pamoja kuujadili, niishangaa kusikia msanii wa aina yako akiimba kwenye beat yenye base lililo off key…that was so irritating. Kwa hadhi yako wimbo huu ninaupa NYOTA 1.

KUMBE

Ilikuwa nzuri hii kitu, moyo wangu ulianza kurudi nyuma tena, kuna genre inakufaa sana wewe mtu, wewe unatakiwa kuijua lakini mimi naweza kusema changanya majaribu, unaniumiza roho na kumbe kupata aina ya muziki wako. Kutokana na kukosa umakini katika vitu vidogo haswa uandishi na adlibbing, wimbo huu naupa NYOTA 4.

KENYA ITADUMU

Nadhani ulikurupuka kufanya wimbo huu, najua una bond nzuri na Wakenya na ilikuwa sahihi kabisa kuwafariji. Nasema ulikurupuka kwasababu haukuimba viziri wala kuandika vizuri, ungetulia vizuri ile ingekuwa zawadi nzuri kwako mwenyewe. Kuna mtu ananiambia haikuwa official release lakini namjibu kuwa kitu kibaya hakitakiwi kwa pro, as long as ni kitu unataka kifikie audience basi u have to give your all kuilinda status yako. Hapa ndipo nilipokushindwa jamaa, nikajiambia sitakufuatilia tena kishabiki kwakuwa unaflactuate sana, sikutaka stress hizi tena. Wimbo huu una NYOTA 1.

FIRE

Siku unaamua kuachia wimbo huu sikupay attention kwasababu nilishakutema, ilinilazimu kuutafuta na kuusukiliza baada ya kukutana na kauli za watu zinazokinzana kwenye mitandao, moyoni nikajiambia kumbe ni kawaida Msechu “kukwaza” mashabiki???!!! Nikaupata na kuamua kuusikiliza kwa sikio la kishabiki tu na hakika si wimbo mbaya sana ila pia sio wimbo mzuri pia. Fire si ni rhumba kabisa? Nikasema huyu mtu mbona hajielewi? Mbona anauchokonoachokonoa muziki? Hivi kwanini hana focus? Nikasema inatosha ngoja nifanye kitu, nikawasiliana na rafiki yangu mmoja kumuambia nia yangu akaniambia as long as nia ni nzuri basi andika, hata kama mapokeo yatakuwa mabaya lakini walau bwana Peter utaamka usingizini na kujievaluate.

Maoni: Haya unaweza kuyachukua ama kuyaacha

Chagua aina moja ya muziki ya kukudefine wewe. Huna haja ya kuprove chochote kwa yoyote kwasababu mwisho wa siku atakayeathirika ni wewe. Kila mtu anakupenda ukiimba aina Fulani ya muziki, fanya audience research ujue wengi wanapenda nini, au fikiri katika aina gani unaweza kuwa na connections nyingi za kuendelea.

Acha complications. Tengeneza muziki rahisi wa kuimbwa na kila kitu, it feels good watu wakiimba nawe wakati unaimba, wewe fujo ni nyingi, nyimbo nyingine intro tu inazungumza kuwa umeamua kuonyesha kwamba unaweza zaidi ya kila mtu, complications hizo ndio zinazaa maneno yasiyo na ulazima ukiadlib, zinazaa makelele (kupayuka), na zinazaa freestyle ambazo wakati mwingine zinakutoa kwenye maana ya wimbo ama kuufanya mwepesi sana kiutunzi.

Jua producer anayekufaa zaidi. Fanya kama nyimbo zoote ulizoachia kuwa ni majaribio ya nani producer mzuri kwako. Kisha fanya uchaguzi wa nani wa kukomaa naye.

Kuwa wewe. Kila wimbo utakaofanya uwe na ladha yako, inaudhi kusikia ladha ya mtu mwingine kwenye sauti yako, u are more than all of them kiuwezo.

Jua primary audience wako. Ni muhimu kujua muziki wako ni kwa ajili ya nani, hii itakurahisishia kuchagua content na maneno kwenye uandishi, hivi sasa hueleweki nani umemtarget na labda ndio maana nyimbo zako hazifiki mbali.

Grow up. Hapa nazungumzia upstairs! Huu sio wakati wa kuwa na sifa sifa, sijui kama ndivyo ulivyo ama vipi ila outlook yako imebadilika sana tangu utoke TPF.

Unaweza kumfollow Kinye kwenye Twitter kwa @kinye42

Credits:Bongo5
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment