(Lyrics) Anna Peter Ft. Hellen - Tunaweza


Mtunzi:Anna Peter
Msanii:Anna Peter ft Hellen
Mtayarishaji:Mr T Touch
Studio:Seductive Rec

TUNAWEZA.
Chorus;
Wanawake Tunaweza, Wasichana Tunaweza
Tunaweza, Tunaweza X2
Kwa pamoja Tunaweza.

VERSE I.
Fanya kazi yako ya mikono,Kwa moyo
Wala hutakosa kupata mapato.
Amka kabla haujaisha usiku
Amka kabla haujaisha usiku
Upendeleo usikundanye
Pia uzuri usikuhadae
Angalia Shamba ukalime
Biashara pia ukafanye

VERSE II.
Kwa mapato yako yote jipatie ufahamu kokote
Mkamate sana elimu usimwache aende zake
Hiyo ni silaha yakooo
Ona madaktari wanawake
Nasema Ona marubani wanawake
Ona viongozi,maraisi wanawake.
Chorus.

Jipambe kwa mavazi ya kujisitiri
Pamoja na adabu nzuri
Na moyo wa kiasi
Utaweza kuwa yeyote
Utaweza kufanya chochote
Unaweza,Utaweza
--------end----------
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment