KUTOKANA NA MACHUNGU YA KUVUNJIKA NDOA BOB JUNIOR, AAMUA KUTUNGIA WIMBO...!


Rais wa Masharobaro, Raheem Ramadhan aka Bob Junior anatarajia kuusema ukweli wake wote uliozunguka maisha yake ya ndoa iliyovunjika kwenye wimbo mpya alioupa jina ‘Ukweli Wangu’.
Akiongea na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia Kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Mbeya, Bob Junior amesema kwenye wimbo mashabiki watamskia alivyoimba kwa hisia kali. “Kuna wimbo unaitwa
UKWELI WANGU mwezi wa pili au mwezi wa tatu nitauachia lakini umeshaisha upo mastered na kila kitu ni wimbo mmoja mkali sana unahusu ukweli wa maisha yangu juu ya mimi na mapenzi yangu yote ni mambo mengi nimeongelea na wimbo wa feeling sana,” amesema.

Katika hatua nyingine, Bob Junior amesema na kuwa booked na u-busy wa majukumu kwa waongozaji) wa video wa
kampuni ya Ogopa Videoz ya nchini Kenya ni sababu kuu iliyochangia video ya BASHASHA kuchelewa kutoka mpaka sasa.

“Video nimepewa nusu demo mpaka sasa hivi, jamaa wamesafiri wapo Marekani kuna project wanaifanya na Wakenya Fulani, wakirudi nadhani deadline next week wamesema watanipa full video, wamenifanya ni delay sana sasa sijui kwamba project yangu watakuwa wameimaliza na kunipa,” amesema muimbaji huyo.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment