Kituko; Wezi wengine Njaa Kweli.. Embu Cheki Huyu Alivyopatikana..

Kuna mwizi aliingia nyumba flani kuiba, mwenye nyumba alikuwa ni hohehahe kupindukia kiasi
ambacho hakuwa na shati wala tshirt, maisha yake yote alikuwa anashinda kifua wazi. mwizi baada ya kuingia ndani akakosa cha kuiba, lakini pembeni aliona chungu kilikuwa na unga
wa muhogo. jamaa akaona sio haba bora achukue chochote; akavua shati lake akalitandika
chini akasogea kwenye chungu cha unga ili aumiminie kwenye shati alilolitandika chini ili
aubebe kirahisi bila kuondoka na chungu, kumbe mwenye nyumba anamuona.

Jamaa alivyogeuza mgongo tu kuchukua chungu, kwa kasi ya umeme mwenye nyumba aliliiba lile
shati na kurudi chumbani fasta, mwizi aliporudi alipolitandaza shati hakulikuta, akaguna kwa
sauti Mhhh!
Mke wa mwenye nyumba akumuuliza mumewe kama naskia kuna mwizi, jamaa akamwambia hakuna mwizi tulale tu! 
Mwizi akapiga kelele hapana mwizi yupo mbona shati langu silioni!
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment