Haya Ndio Maneno ya Mzee Chilo kwenda kwa wasanii wasioshiriki kwenye matatizo ya wasanii wengine

MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Ahmed Ollotu ‘Mzee Chilo’ amewatolea uvivu wasanii wasiopenda kushirikiana na wenzao katika matatizo na kuwaonya kuwa tabia hiyo si nzuri kwani ipo siku itawaponza.

 Chilo aliyejizolea heshima na umaarufu mkubwa katika fani hiyo, alikiri kuwa wasanii wengi wamekuwa wakijitenga na wenzao wakati wa matatizo jambo ambalo linakera na kuumiza.

Msanii huyo alisema hakuna binadamu anayejua hatima ya maisha yake hapa duniani, hivyo ni vyema kuishi katika mwenendo ulio mzuri, kwani watu wote ni udongo na mavumbini watarejea.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment