DJCHOKA: HIZI NDIZO SABABU ZANGU KWANINI NIMEPUMZIKA KAZI YA UDJ


Leo naomba niwatangazie wadau wangu na mashabiki wote waliokuwa wakinipenda kipindi nikiwa nawadj wasanii wa hapa nchini na hata wale wasanii waliokuwa wakitoka nje ya bongo. Natangaza rasmi kupumzika kazi hii ya uDJ niliyoanza nayo toka 2005 mpaka leo, sababu za kupumzika nimeona nipumzishe uDJ niendelee na kazi inayoniingizia kipato nazungumzia website yangu hii tokea ikiwa ni blog.

Kazi ya kudj wasanii ni kazi fulani nzuri lakini ni ngumu sana usipokuwa na hobby nayo, nimeifanya kazi hii kwa mapenzi yangu mwenyewe yakupenda mziki na sikuwahi kulalamika mslahi ninayoyapata kwasababu niliifanya kazi hii kwa mapenzi yangu mwenyewe hata napokuwa jukwaani nilikuwa nafurahia sana. Lakini kwa kuwa kazi hii ya kuandika habari na kuonyesha kazi za wasanii wa hapa nchini ndio inayonilipa vizuri basi naona sina budi kupumzisha kimoja ili niendelee na kimoja

Baada ya kupumzisha kazi yakudj kwenye majukwaa na kuwadj wasanii sasa nitakuwa naendelea na kazi yakuvumbua vipaji vya wasanii pia nitaendelee na mix tape zangu kama kawaida. Msanii atakayenihitaji sasa hivi basi ujue itakuwa kazi yakwenda kupiga picha show zake au kurecord show zake TU akiwa jukwaani. Mbali na hapo nitaendelea kupromoti mziki wa nyumbani na wasanii wake mpaka mwisho wangu. Nawakaribisha madj wadogo ambao mlipenda kuwa madj wa wasanii na hamkujua jinsi yakuanzia, nitawashauri na pia nitawafundisha njia za kuwadj wasanii hususani wasanii wa Hip Hop na Bongo Fleva unacheza nao vipi unapokuwa nao jukwaani.
Nawapenda sana wadau wote wa DJCHOKA MUSIC kwasababu bila nyie hakuna mimi
ONE
DJ CHOKA
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment