DIAMOND PLATNUMZ AONGELEA NDOA YAKE NA VJ PENNY | SOMA ALICHOKISEMA HAPA

SIYO siri kwamba wapenzi wasio na kificho, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Penny Mungilwa wana malengo ya kuja kuishi kama mke na mume lakini maajabu ni namna mwanamuziki huyo alivyopanga sherehe ya ndoa yao iwe siku ikifika.
.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Diamond alisema kuwa yamekuwepo maneno ya chinichini kuwa ameshatoa mahari na siku si nyingi ataingia kwenye maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba kila kitu kinafanyika kwa umakini na mashabiki watajulishwa hatua kwa hatua.

“Suala la ndoa yangu nalifanya kwa umakini sana, watu wawe na subira tu ila wanachotakiwa kujua ni kwamba nina plani za kuifanya sherehe ya ndoa yangu kwenye Uwanja wa Leaders Club, pale Kinondoni na watu wataingia kwa kiingilio kisichopungua shilingi elfu kumi. Itakuwa ni ndoa ya Wasafi bana,” alisema Diamond.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment