JAQUELINE WOLPER:PENZI LANGU NA DALLAS ILIKUWA NI FILAMU TU.

Jack Wolper
Wolper Gambe mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI nguli katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ ametoa mpya pale aliposema kuwa uhusiano wake na Dallas uliotikisa kwa kuripotiwa sana na vyombo vya habari ulikuwa kama tamthilia ya kusadikika na hakukuwa na penzi la kweli, akiongea na FC mwanadada huyo anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo alidai ukikutana na mwongo igiza.

.
Jack Wolper
Wolper Gambe katika pozi
Dallas
Huyu ndio Dallas aliyeingia chaka kwa mtoto wa kichaga.
Jack Wolper
Wolper Gambe enzi akiwa katika filamu ya Ndoa yake na Dallas.
“Japo mara nyingi sipendi kuongelea sana kuhusu mahusiano yangu zaidi ya kazi yangu ya uigizaji, lakini penzi langu na Dallaz ilikuwa ni filamu tu, si unajua mimi ni mwanamke ninayehitaji kupendwa na kuthaminiwa na ninahitaji kupendeza na kumwamini mtu sasa ukikutana na mtu asiyeeleweka na mjuaji na wewe unamtengenezea Script tu maisha yanaendelea,”anasema Wolper Gambe.
Wolper siku za nyuma akiwa na Dallaz pia alitangaza kubadili dini na kutoka dini yake ya awali Ukristo na kuwa Muislamu lakini baada ya filamu hiyo kumalizika amerejea katika dini yake ya awali na hapendi hilo liongelewe kuhusu suala la imani yake, ukitaka kuongea na Wolper Gambe basi muulize jinsi gani anavyopiga mzigo katika filamu na si maisha yake kwa undani.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment