UZINDUZI WA MARCO CHALI FOUNDATION NA EPIC OPEN MIC WAACHA HISTORIA DAR MWEMBE YANGA


Wasanii Daimond na Ney wa Mitego kwenye stage jana pande za Mwembe Yanga Temeke
GodZilla aka  King ZiZi akifanya yake
Mabeste
 Madee
Produza wa Mj Records ,Marco Chali akitoa maelezo kuhusu Foundation yake na Epic Open Mic
Ramadee na Mapacha
Mshindi wa EBSS Walter Chilambo akiimba kwenye tamasha hilo.
Katika kuelekea msimu wa sita wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imezindua Epiq Open Mic ikiwa ni nafasi nyingine kwa vijana wenye vipaji vya muziki kuonyesha vipaji vyao kabla usaili wa Epiq Bongo Star Serach haujaanza.

Epiq Open Mic inatarajiwa kuwapa nafasi vijana kujifunza misingi ya muziki kutoka kwa mmoja wa watayarishaji wa muziki maarufu zaidi nchini, Marco Chali.

Marco Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. Trinity kutokea Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na wengine wengi.

Tamasha hilo la Epiq Open Mic, ambalo ni la bure lilizinduliwa rasmi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke tarehe 26 ya mwezi huu ikisindikizwa na wakali kibao wa Bongo flavor kama Diamond Platnumz, Madee, Godzila, Ney wa Mitego, Mabeste na Mrap.

Baada ya uzinduzi wa tamasha la Epiq Open Mic Mwembe Yanga tamasha hilo litaendelea kila jumamosi kwenye makao makuu ya Zantel likiwapa nafasi vijana kujisajili na kurekod sauti zao.

Vijana watakaorekodi sauti zao watapigiwa simu na timu ya watayarishaji wa muziki chini ya Marco Chali pamoja na wanamuziki ili kuwapa ushauri wa namna ya kuboresha muziki wao zaidi.

Zantel imejipanga kutumia fursa hii kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao, kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisisitiza Khan.

Epiq Open Mic pia inatarajia kuwapa fursa ya kurekodi baadhi ya vijana watakaokua na vipaji.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment