FILAMU INALIPA KULIKO UTANGAZAJI- IRENE PAUL.

Irene Paul
Irene Paul mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI wa kike Irene Bahati Paul anayefanya vinzuri katika tasnia ya filamu Bongo amedai kuwa ameachana na kazi ya utangazaji baada ya kubaini kuwa filamu inamlipa kuliko fani ya utangazaji aliyekuwa akifanya na kubaini kuwa maslahi kwake ni madogo tofauti na alipojiunga na uigizaji kwa muda mfupi tu faida kaiona.
Irene Paul
Irene Paul akiwa katika pozi la picha.
Irene Paul
Irene Apul katika pozi la kufa mtu
“Kwangu mimi filamu inanilipa na imekuwa nimeamua kuachana na kazi nyingine zote ili niwe makini na kazi ya uigizaji ambayo naona maslahi ya moja kwa moja na ni kazi ambayo ninaipenda sana imenikutanisha na watu mbalimbali marafiki pia imebadilisha maisha yangu napata ninachohitaji bila wasi wasi,”anasema Irene. Irene alianza kutangaza katika televisheni ya C2C na baadae Clouds Tv na kuachana na kazi hiyo ya utangazaji kuingia katika uigizaji baada ya kukutana na Ray na kupewa nafasi ya uigizaji, msanii huyo pia amewashukru Zamaradi Mketema kwa kumshauri kuingia katika uigizaji kwani aliona kipaji chake.
Msanii huyu ameshiriki filamu na wakongwe katika tasnia ya filamu Kanumba na Ray, filamu alizoigiza ni I hate my Birthday, Kibajaji, More than Pain, Kalunde filamu aliyoitengeneza mwenyewe na
imeonekana kufanya vizuri sokoni.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment