UHURU KENYATTA, Atangazwa Rais Wa 4 Wa Jamhuri Ya KENYA... RAILA ODINGA Kwenda Mahakamani

Hatimaye aliekuwa mgombea wa kuwania kiti cha uraisi nchini Kenya Bw. Uhuru Kenyatta amemshinda mpinzani wake Bw. Raila Odinga kwa jumla ya kura 6,173,433 na kutawazwa Rais wa Jamhuri Ya KENYA.
Raila Odinga ambae ndiye alikuwa mpinzani mkuu, alipata jumla ya kura 5,340,546 kutoka chama pinzani.
Jumla ya kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa kwa nafasi ya uraisi ni 12,336,667 kutoka katika majimbo yote ya uchaguzi 291.
Kura zilizoharibika zikiwa ni 108,975 na hivyo kubaki 12,222,980.
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.


Habari zaidi zinadai kuwa ushindi wa Uhuru Kenyatta umesababisha mpinzani wake ambae alikuwa ni waziri mkuu wa zamani Raila Odinga kuamua kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo huku pia akilaumu kuwa IEBC imerudia makosa yake ya mwaka 2007.
IEBC ni tume inayoendesha zoezi zima la uchaguzi nchini Kenya.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment