PAPA BENEDICT XVI AJIUZULU

Kwa habari zilizotufikia hivi punde zinasema Papa Benedict XVI (85) ajiuzulu wadhifa wake.
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa wadhifa huo kufanya hivyo kwa miaka 600 iliyopita, Papa Benedict XVI amejiuzulu kwa sababu aliyoitoa mwenyewe kuwa ni kutokana na umri.
Na ataachia madaraka February 28 na Papa mwingine atachaguliwa Machi. ''Baada ya kutafakari umri wangu sasa hainiruhusu kuendelea katika wadhifa huu kutokana na mabadiliko ya kiimani kwa mujibu wa Mtakatifu Peter...'' alisema Mtakatifu Benedict (85).
Papa wa mwisho kujiuzulu alikua ni Papa Gregory ambaye alijiuzulu mwaka 1415 kutokana na mgawanyiko wa kidini katika nchi za magharibi

0 comments: