BALOTELI APIGWA KADI NYEKUNDU

BALOTELI APIGWA KADI NYEKUNDU
Apigwa kibuti kwa Trey Songz
Tabby Brown

Mchezaji mtukutu wa timu ya Mancherster City ya nchini Uingereza  Mario Baloteli, ameuanza mwaka 2013 kwa kuandamwa na mabalaa kila kukicha. Safari hii Baloteli ameachwa akiwa amechanganyikiwa baada ya kupewa kadi nyekundu na aliyekuwa mpenzi wake mwanamitindo wa klabu ya usiku ya playboy Tabby Brown na hatimaye kalihamisha penzi kwa mwanamuziki wa RnB na mtayarishaji muziki Mmarekani Trey Songz. 
Balotelli kama vile anafungasha virago vyake baada ya kutoswa

Mshambuliaji huyu raia wa Italia mwenye umri wa miaka 22 ambaye wiki hii alipata balaa lingine la kukwaruzana na meneja wake wakati wakiwa mazoezini.

Imeelezwa na baadhi ya mashoga wa karibu na Tabby wakisema "Imemchanganya sana na amechukizwa kwani alikuwa amekasirika sana na alijaribu kumbembeleza lakini wapi, inaonekana Balotelli hajawahi kuachwa na mwanamke katika maisha yake"

Mario Balotelli na mpenzi wa zamani aliyezaa nae mtoto wa kwanza Raffaella Fico. 
Tabby Brown akiwa na mpenzi wake mpya Trey Songz

Wambea hao waliendelea kuchonga na kusema "alikuwa hamjali na amechoshwa na tabia zake kuwa na wanawake wengi".
Mapenzi yao ya miezi saba yalikuwa yamefikia ukingoni baada ya Baloteli kufumwa akiwa ametumiwa meseji kwenye simu yake na mpenzi wake wa zamani Raffaella Fico ambaye aliishapewa mimba na Baloteli, na alipomuuliza akasema "ni rafiki yangu tu"

Tabby na Balotelli wote walipoulizwa walikataa kukubali kutengana kwao.

Mshike mshike Balotelli na Roberto Mancin
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment