SHUKRAN NA UJUMBE KUTOKA KWA DAYNA [MKALI WAO].


Mambo vp ndugu zangu. Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia maandalizi mema ya mwaka mpya. Mungu atupe nguvu na neema zaidi ktk mwaka 2013.  Mwaka 2012 tutaukumbuka kwa mengi yapo mema na mabaya. Naomba nikuombe radh wewe kwa lolote ambalo niliwah kukukosea, nawe kama ulinikosea sina tatizo nawe tangu sasa. pia naomba nitoe shukrani zangu kwa wote waliohusika ktk mafanikio yangu ya kimuziki.  Naamini wengi mlikuwa mstari wa mbele ktk kunishauri, kunipongeza nahata kunikosoa nilipokosea. Shukrani nying zwafikie radio presenter, dj's,  radio na tv zote tz na  Afrika naamini bla nyinyi kuzicheza nymbo zang Basi nisingefika hapa. Waandaz wa magaazeti mlikuwa mstari wa mbele ktk kuona nafika mbali kwa kuandika habari zangu na kufika hata vjijini. Nachukua fursa kuwashukuru pia. 

Blogs mbalimbali. Mlikuwa mstari wa mbele kwakuandka habari na kupost hata baadh ya show zangu ambazo mmenipa heshma ya kufika mbali zaid na kusikika hata nje ya nch mchango wenu ni mkubwa  japo siwez kuwataja wote. Pia Requester wa media cna cha kuwalipa nawashkuru sana sana na ntabaki kuwaheshmu kwani mmetoa mchango mkubwa sana kwa kuomba nymbo zangu media na zikachezwa Na amini ni mchango mkubwa sana ktk game hasa kwetu wasanii Ntabaki kuwaheshimu na kuwathamini siku zote. Bila kuwasahau wasanii wenzangu walikuwa nami bega kwa bega ktk  kunishauli na kunisaidia kwa chochote.Pia ma dj wa club mbalimbali, mmekuwa chachu ya mzk wangu pale mlipoonesha ushirikiann wenu kwangu. 

Pia Waandaaji wa (show) matamasha  madogo na makubwa nawashukuru sana sana kwa kuniamini na kukubali kufanya kazi na mm Siwasahau maproducers wa video na  Audio  na studio mbalimbali kwa kunifanyia kaz za uhakika na jamii ikanikubali kwa kazi hzo. Wote kwa pamoja naamini sasa ni kama ndugu. Nawaomba muonyeshe tena moyo huwo na mwaka ujao na mingine kwani kaz nzur ni yenye kushirikiana. Msisite kama ntawakosea naomba msisite kunikanya na kunisamehe. Napenda wote na kuwajali. Nawatakia  mwaka mpya. Ts me.              
 Dayna Nyange (mkali wao)
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment