Wamarekani wachukizwa na kitendo cha Chris Brown kuvaa kama Taliban kwenye Halloween party ya RihannaChris Brown (katikati) akiwa na washkaji zake
Juzi Rihanna aliandaa party ya Halloween huko West Hollywood na kukaribisha mastaa kibao akiwemo swahiba wake Chris Brown.
Chris ndiye aliyezua mjadala kutokana na kuvaa kama wanamgambo wa Taliban. Akiwa amevaa nguo hizo Chris alivaa pia mkanda wa risasi kifuani mwake pamoja na kushikilia machine gun huku akipewa kampani na washkaji zake waliokuwa wamevaa kama yeye.
Aliweka picha hiyo kwenye mtandao wa Instagram na kuandika “Ain’t nobody F**king wit my clique!!!!”

Mastaa wengine waliohudhuria party hiyo ni pamoja na Flo Rida, Paris Hilton, na staa wa Olympic Lindsay Vonn.
Baada ya watu kumshambulia Chris kwa kitendo hicho cha kuwaunga mkono magaidi mama yake Joyce Hawkins alimtetea mwanae kwa kuandika, “HALLOWEEN IS FOR FUN NOTHING MORE THAN JUST FUN. GET A LIFE PLEASE.”
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment