Kimenuka Tena:Mhariri wa Gazeti la Business Times Apigwa Risasi

Mnaku Mbani Lukanga (Mhariri wa gazeti la Business Times ) akiwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili leo asubuhi alipohamishwa kutoka hospitali ya Temeke alikolazwa jana mara baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi hapo jana usiku katika mtaa wa Lugoda akiwa anaelekea nyumbani kwake Mbagala usiku wa saa mbili jioni. Katika tukio hilo, alikuwa na abiria wenzake 6 ambao nao walipigwa risasi. Baadhi yao walitolewa risasi na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Mnaku alipigwa risasi juu yo mdomo na risasi hiyo kutokea kwenye shavu lake la kushoto. Bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment