Exclusive: Barnaba azungumzia sababu za kushindwa kuhudhuria show ya Africa Unplugged
Mwishoni mwa mwezi August mwaka huu Barnaba alikuwa msanii pekee wa Tanzania aliyechaguliwa kwenda kuperform kwenye show kubwa iliyopewa jina la Africa Unplugged jijini London Uingereza.

Barnaba ameiambia Bongo5 kuwa sababu za kushindwa kuhudhuria show hiyo ni kukosa visa ya kwenda nchini Uingereza.

“Sikwenda kwasababu passport yangu ilicheleweshwa kutokana na ubalozi wa UK ambao uko Tanzania makao makuu yake ni Nairobi kitu ambacho mimi kama mtanzania sikukipenda pia why ubalozi wetu wa UK uwekwe Nairobi? Kwanini wa Nairobi usibaki Nairobi wa Tanzania usibaki Tanzania? Hicho ni kitu ambacho kimenidisappoint pia. Kusubiri visa yangu ambayo nilitakiwa nisubiri ilibidi nisubiri siku 14 na siku za safari zilibaki saba kwahiyo nilichelewa siku saba mbele yake, ilibidi niikose show. Iliniathiri sababu ilikuwa bonge la opportunity inawezekana ningepata mlango mwingine na kunifanya kuwa mkubwa. Nilitegemea kulipwa lakini hata kama nisingelipwa, malipo yangu ya kupata nafasi kubwa zaidi ya kazi nyingine nafikiri ilikuwa kubwa kuzidi hata ile percent ambayo ningepata.

Kuhusu kuchelewa kufanyika kwa collabo yake na Fally Ipupa

Collabo ya mimi na Fally Ipupa ipo lakini nafikiri connection kidogo imekuwa ngumu kutokana na mtu mwenyewe ni mkubwa amekuwa na mambo mengi ana tour nyingi na mihangaiko inayonitinga hapa Tanzania ni mingi kwahiyo sina cha kusema sana kwa sasa mpaka nitakapoifuatilia tena hii issue lakini mawasiliano yapo na connection kubwa ipo.

Wakati huo huo Jumanne ijayo Barnaba ataachia wimbo mpya alioupa jina la Sorry ambapo amesema: “Ni nyimbo yangu mpya kabisa ambayo naamini inaweza kubadilisha soko la muziki wa kitanzania. Nyimbo imetengenezwa na watu wengi producer ni Imma the Boy imetengenezwa pale THT , mwandishi ni mimi mwenyewe Barnaba lakini watu wengi wameshiriki.”

Amewataja wengine walioshiriki kuwa ni pamoja na Ditto, Mwasiti, Waziri Njenje, Kardinal Gentle.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment