‘BADRA’ KUJA NA NGOMA MPYA, AAMUA KUMSHIRIKISHA MSANII MKUBWA WA HIP HOP…!!

MSANII wa filamu pekee ambaye anafanya muziki wa Hip Hop Tanzania Latif Idabu ’Badra’, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa leo anatarajia kuingia studio kwa ajili ya kurekodi ngoma yake mpya, ingawa aliweka wazi kuwa bado hajajua aipe jina gani hadi sasa lakini pia anatarajia kumshirikisha msanii mkubwa wa Hip Hop.

Msanii huyo ameweka utofauti kidogo kwani wasanii wengi wanaotokea kwenye filamu wanafanya muziki unaofanana, kitu ambacho kinafanya watu wanashindwa kuwatofautisha na wanahisi wanaingia kwenye tasnia ya muziki kwa lengo la kutupiana maneno badala ya kuitendea haki tasnia hiyo.

0 comments: