‘JACKLINE WOLPER’ ADAI KIWANGO CHAKE WANAKIJUA MASHABIKI WA KAZI ZAKE, AKANA KUACHWA NA ‘DALLAS’…!!

BAADA ya msanii Irene Uwoya kudai kuwa msanii mwenzake Jackline Wolper hana kiwango cha kuweza kushiriki naye kwenye filamu moja, naye Wolper amejibu mapingo kuwa hata yeye haitaji kucheza naye kwani anaamini kiwango chake si cha mdomoni bali mara zote anakionesha akiwa kazini na hata mashabiki zake wanajua hilo.

Mtandao wa DarTalk ulitumia nguvu ya ziada kutafuta Wolper ambaye mara kadhaa simu yake ilikuwa imezimwa na baada kupatikana msanii huyo alidai yuko bize ambapo aliamua kumtumia rafiki yake wa karibu ili kujibu hoja, ambapo alidai kuwa hawezi kuzungumza chochote kwani wanaosema yeye hana kiwango hawamjui na wanamuona juu juu lakini hawajawahi kushiriki naye kwenye kazi ambayo inaweza kutoa majibu yote.

Rafiki huyo ambaye hata hivyo alikaa kujitambulisha jina, alidai alichoambiwa akijibu ndicho anachokitoa, ambapo aliongeza kuwa kauli ya Uwoya haimshtui na ataendelea kusimama imara katika kila kazi anayotoa kwa lengo kuwapa ujumbe mashabiki wke.

“Kwangu siwezi kujibu kauli za mtu ambaye hana uwelewa wa nini anachikisema najua ni kwamba wanaoweza kutoa kauli kama hizo ni mashabiki na wapenzi wa kazi zetu, hivyo nawaomba wadau wa wangu wasimsikilize mtu ambaye anakaribia kupotea kwenye tasnia,”.

Hata hivyo baada ya kuachana na rafiki huyo mwandishi wa habari alizungumza tena Wolper, ishu iliibuka upya ni kwamba baada ya kudaiwa kuwa wameachana na mpenzi wake Dallas na amepokonywa mkoko wa wenye thamani ya sh 175, alikana habari hizo na kudai kuwa yeye mwenyewe hajatamkiwa kuwa ameachwa.

“Hizo habari hazina ukweli si unajua watu wakiamua kutoa ishu za uongo wanatoa ili tu mtu aonekana mbaya, lakini najua nafasi yangu ni ipi ” alidai Wolper.
Share on Google Plus

About Bachema

Blog hii inamilikiwa na Bachema Media,Kwa Biashara na Matangazo Wasiliana nasi kwa Tigo:0717342094,Email.bachemao@gmail.com.kama una wimbo pia unaweza kutuma kwenye email.bachemao@gmail.com.Karibu utangaze nasi kwa Bei Nafuu Kabisa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment